ZINAZOVUMA:

Mahakama yatupilia mbali kesi kupinga ushindi wa Rais Nigeria

Mahakama nchini Nigeria imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na upinzani kupinga...

Share na:

Mahakama nchini Nigeria imetupilia mbali rufaa ya kesi iliyomuingiza madarakani Rais Bola Tinubu na kuidhinisha matokeo ya kura zilizopigwa baada ya kuona kuwa kesi hiyo haikuwa na mashiko.

Rais Tinubu alichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Februari mwaka huu, ambapo wagombea walioshindwa walienda mahakamani kupinga matokeo hayo wakisema uchaguzi ulikua na dosari.

Atiku Abubakar mgombea kutoka chama cha People’s Democratic Party, na Peter Obi wa Labour Party, walikuwa wamedai ukiukaji wa sheria za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kutokutumika mashine za kielektroniki kujaza matokeo ya vituo vya kupigia kura.

Aidha uamuzi huo unatarajiwa kupelekwa katika Mahakama ya Juu, ambapo Abubakar na Obi wanaweza kukata rufaa ndani ya siku 60.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa Mahakama ya juu haijawahi kutoa uamuzi wa kutengua matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Nigeria tangu nchi hiyo irejee kwenye demokrasia kutoka kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya