Taarifa kutokea nchini Congo zinaarifu kuwa Kundi la waasi la M23 Movement (M23) linatarajiwa kujiondoa katika maeneo ya jimbo la Nord Kivu mashariki Nchini humo.
Ifahamike kuwa Wanajeshi wa Kikosi cha Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) watachukua maeneo ambayo waasi hao wa M23 walisalimu amri, ambapo kuibuka kwao kwa mara nyingine mwishoni mwa 2021 kumesababisha vifo vya mamia na maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Mpatanishi maalum wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uhuru Kenyatta, alisema tarehe 4 Aprili kwamba M23 watajiondoa katika maeneo zaidi ya Nord Kivu kufikia leo.