Mshambuliaji wa Kibelgiji aliyekuwa anakipiga katika Klabu ya Chelsea, Romelu Lukaku, amejiunga rasmi na ligi ya nchini Italia, Serie A, na ataichezea Klabu ya AS Roma.
Lukaku amekamilisha uhamisho huo wa mkopo baada ya Chelsea na AS Roma kufikia makubaliano ya dola milioni 8.7 kwa mchezaji huyo kuitumia timu hiyo ya Italia kwa msimu mmoja.
Pia Lukaku mwenye umri wa miaka 30 atalazimika kupunguza mshahara wake anaolipwa kwa sasa.
Awali, Inter Milan ilitaka kumsajili baadaye ikajitoa katika mchakato, Juventus nayo ilionesha nia lakini mashabiki wa timu hiyo waliandamana wakidai hawamtaki. Aidha, Lukaku alikataa ofa ya kuhamia Al-Hilal ya Saudi Arabia.