Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu OCHA imesema inawasiwasi na mabwawa mengine mawili nchini Libya huenda yakapasuka na kusababisha maafa zaidi.
Mabwawa hayo ni Jaza ambalo kwa kiwango kikubwa liliharibu vibaya jiji la Darna na Benghazi na Bwawa la Qattara karibu na Benghazi.
Shirika hilo la Umoja wa mtaiafa limesema kumekuwa na “ripoti kinzani” kuhusu uimara wa mabwawa hayo.
Mabwawa yote mawili yalikuwa katika hali nzuri na kufanya kazi, kulingana na mamlaka ya libya lakini kulingana na taarifa za hivi karibuni inaonesha kuwa huenda yakapasuka na kusababisha mafuriko mengine.