ZINAZOVUMA:

Kim Jong Un amaliza ziara yake ya siku sita Urusi

Raisi wa Korea kaskazini Kim Jong Un amemaliza ziara yake...

Share na:

Raisi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ameondoka nchini Urusi usiku wa kuamkia leo Jumatatu Septemba 18, 2023 baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita, ambayo ililenga kuimarisha uhusiano wake na Rais Vladimir Putin.

Katika ziara hiyo siku ya jana Jumapili, Kim alikitembelea Chuo Kikuu cha Mkoa wa Primorye kabla ya kusubiri treni yake ya kisasa, kuanza safari ya kurejea Korea Kaskazini.

Ziara hiyo ya Kim huko upande wa mashariki mwa Urusi ilianza Jumanne iliyopita kwa mkutano wa kihistoria na mwenyeji wake Rais Putin na kisha kuitembelea kambi ya jeshi la nchi hiyo ya bahari ya Pasifiki.

Kabla ya Kim hajaondoka, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, alisema Moscow itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Korea Kaskazini chini ya misingi ya haki na usawa.

Mataifa ya magharibi ikiwemo Marekani yamesema ziara ya kiongozi huyo ilikuwa na na dhima ya kujadili uwezekano wa Korea Kaskazini kuipatia Urusi silaha.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya