ZINAZOVUMA:

Kenya: Maandamano kila Jumatatu na Alhamisi.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya ametangaza kuendelea kwa maandamano nchini...

Share na:

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesema kila siku za jumatatu na Alhamisi watakua wakiandamana kufuatia matakwa ya wananchi wake.

Akizungumza siku ya leo Raila Odinga amesema maandamano yaliyoanza siku ya jana jumatatu hayataisha mpaka pale serikali ya William Ruto itimize mahitaji Yao.

Licha ya kutishiwa na polisi, kupigwa kwa mabomu ya machozi na baadhi ya waandamanaji kukamatwa na jeshi la polisi nchini Kenya, Raila Odinga amesema hawatarudi nyuma wala kukata tamaa.

Ikumbukwe kuwa Raila Odinga ni kiongozi wa Chama cha Azimio ambae aligombea uraisi dhidi ya Raisi mteule William Ruto ambapo Odinga alipinga matokeo ya uchaguzi huo na kwenda mahakamani japo huko nako hakufanikiwa.

Kenya kwa sasa inapitia machafuko kutokana na maandamano yanayofanyika kupinga uongozi wa Raisi William Ruto ambapo raia wanalalamika maisha yamekua ghali.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya