ZINAZOVUMA:

Kenya kuongeza mtaji katika benki ya AFDB

Rais Ruto atangaza kuongeza hisa kwenye benki kubwa tatu za...

Share na:

Kenya imetangaza mpango wa kuongeza hisa katika benki kubwa tatu za afrika, ikiwemo Benki ya Maendeleo Afrika (AFDB), kwa kuwekeza karibu Dola za marekani milioni 100.

Benki zitakazonufaika na mpango huo wa Kenya kuongeza hisa ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki ya Afrexim na Benkiya Biashara na Maendeleo (TDB).

Mpango huo ulisemwa na Rais William Ruto katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika nchini Kenya katika jiji la Nairobi.

Pia Rais Ruto aliongeza kwa kusema kuwa “kama Mataifa ya Afrika tunatakiwa kuyaamini mashirika yetu ya kifedha na kuwekeza huko, ili watu wan je nao wayaamini na kuwekeza fedha zao katika mashirika yetu”

Sababu kubwa aliyotaja Rais Ruto kumpa msukumo wa kuongeza mtaji kwenye benki hizo, ni faida kutokana na gawio lililopatikana kutokana na kuwa mwanahisa wa benki hizo.

Mbali na uwekezaji huo pia Kenya inatarajia kuwekeza dola za marekani milioni 20, kwenye mikipo ya masharti nafuu kupitia benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Uwekezaji huu wa pili utaumika zaidi katika kutoa mikopo kwa mataifa yenye hali tete kiuchumi barani Afrika.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya