ZINAZOVUMA:

Kenya kujenga mtambo wa nyuklia kuanzia 2027

Serikali ya Kenya imetangaza mpango wake wa kujenga kinu cha...

Share na:

Serikali ya Kenya imesema itaanza kujenga kinu cha nyuklia kuanzia mwaka 2027 ambacho kitakua na Megawati 1,000 ambao ni sehemu ya mpango wa nchi kuhamia kwenye nishati safi na kuongeza uzalishaji wa kawi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati ya Nyuklia (NuPEA) Justus Wabuyabo aliliambia gazeti la Business Daily la Kenya kwamba shirika hilo kwa sasa linafanya tathmini ya eneo na kukamilisha maandalizi ya kufungua zabuni za ujenzi wa kiwanda hicho.

Wabuyabo alisema kuwa kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la pwani ya Kenya kwa muda wa miaka sita hadi kumi, huku mtambo wa kwanza ukianza kufanya kazi mwaka 2034 .

Baadhi ya Wakenya wamekosoa mpango huo wakidai kuwa kiwanda cha nyuklia si cha lazima na nchi haina uwezo wa kushughulikia taka za nyuklia.

Kwa sasa, Afrika Kusini ndiyo nchi pekee ya Afrika inayozalisha nishati ya nyuklia kibiashara.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya