ZINAZOVUMA:

Iran yajenga urafiki na Zimbabwe

Iran na Zimbabwe zimeingia makubaliano na kutia saini mikataba 12...

Share na:

Iran na Zimbabwe zimetia saini makubaliano 12 ambayo yatenda kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.

Hayo yamefanyika wakati wa ziara ya Rais wa Iran Ebrahim Raisi alipotembelea Zimbabwe siku ya jana na kukaribishwa kwa shangwe na Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa.

Raisi wa Iran amekuja Afrika katika ziara yake ya nchi tatu barani humu ambapo lengo lake ni kukuza uhusiano baina ya Taifa lake na mataifa ya Afrika.

Raisi Mnangagwa amesema Iran ni rafiki wa Zimbabwe hata wakati walipoenda vitani Iran alikua rafiki yao.

“Mkimuona yeye mmeniona mimi, mkiniona mimi mmemuona yeye” miongoni mwa kauli alizoongea Rais Emmerson Mnangagwa mbele ya halaiki ya watu wa Zimbabwe waliojitokeza kumpokea Rais wa Iran.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya