ZINAZOVUMA:

IDA yawafunda vijana.

Taasisi ya Islamic Development Agency kwa kushirikiana na Taasisi ya...

Share na:

Taasisi ya Islamic Development Agency IDA imefanya semina maalumu kwa vijana kwa kushirikiana na Taasisi ya vijana wa kiislamu TAMSYA siku ya jana tarehe 10 Aprili 2023.

Semina hiyo ambayo iliambatana na iftari ya pamoja iliwakutanisha viongozi wa vyuo mbalimbali ndani ya Dar es salaam pamoja na pwani ambao walihusiwa mambo mengi na wazungumzaji waliotoa mada mbalimbali.

Miongoni wa wazungumzaji waliokuwepo ni pamoja na aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali C.A.G prof Mussa Assadi, prof Mohammed Bakari, Dr Pazi Mwinyimvua, Mkurugenzi wa Amana Benki Abubakar Athumani na wengine wengi.

Katika mengi yaliyozungumzwa katika hadhara hiyo ni pamoja na changamoto za ajira kwa vijana wa kiislamu na nini wafanye ili kukabiliana na changamoto hizo, lakini utambuzi binafsi na nini kijana anatakiwa afanye.

Aidha Raisi wa TAMSYA Kassimu Ibrahim, amewashukuru IDA kwa kushirikiana nao katika kuandaa warsha hiyo na kuomba ziendelee kuwa nyingi zaidi kwani zimelenga katika kumkomboa kijana.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya