Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha nchini Uingereza Rachel Riley amesema kuwa ataacha kuiunga mkono klabu ya Manchester United ikiwa mshambuliaji Mason Greenwood atasalia katika klabu hiyo.
Manchester United inasema hakuna uamuzi wowote ambao umechukuliwa mpaka sasa kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo.
Greenwood mwenye umri wa 21 alikuwa akituhumiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo la kujaribu kubaka na kushambulia, hata hivyo huduma ya mashtaka ilifuta mashataka yote mawili.
Aidha mtangazaji mwenza wa Riley aliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa wote wameona na kusikia na wanaitaka klabu ichukue hatua la sivyo hawataiunga mkono Manchester United.
Tangazo kutoka kwa Manchester United kuhusu Greenwood lilitakiwa kutoka kabla ya mechi ya Jumatatu ya Ligi Kuu dhidi ya Wolves lakini halikutoka.