ZINAZOVUMA:

Girkin, Hasimu wa Putin Kisiasa

Kamanda Igor Strelkov maarufu kama Girkin, aamua kusaidia Urusi kisiasa,...
Igor "Girkin" Strelkov katika vita ya Crimea
Girkin katika Operesheni za vita ya Crimea

Share na:

Kamanda wa Urusi anaepinga msimamo wa Taifa hilo juu ya maamuzi ya vita dhidi ya Ukraine, ameshikiliwa kwa kumtuhumu Rais putin na viongozi wengine wa kijeshi.

Tuhuma hizo ni juu ya kutumia kutumia nguvu kubwa ya kijeshi kuipiga Ukraine.

Igor Strelkov ni Kamanda wa zamani wa jeshi la Urusi, aliyepigana katika vita na Ukraine katika eneo la Crimea mwaka 2014, Pia ndie mratibu mkuu wa kikundi cha wapiganaji kinachoshikilia eneo la kaskazini mwa Ukraine.

Mwezi Mei Girkin alitambulisha kikundi chake cha “wazalendo wenye hasira” chenye mlengo wa kisiasa kwa ajili ya kuikomboa nchi ya Urusi.

Mke wa Girkin ametoa taarifa akisema kwamba hajui mumewe alipo kwani alichukuliwa na wawakilishi wa kamati ya uchunguzi akapelekwa kusikojulikana.

Wakili wa Girkin, Alexander Molokhov alisema kuwa mteja wake anashikiliwa na vyombo vya usalama nchini humo, na anapambana kuhakikisha anakutana na mteja wake huyo.

Kwa upande mwingine wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini urusi, wanasema kuwa Girkin amekuwa mwiba uliokuwa ukitafutiwa dawa muda mrefu. Na sasa serikali ya Putin imepata sababu ya kumuweka katika kikaangoni.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya