Kichanga cha kike chaokolewa kikiwa hai kutoka katika tumbo mama wa kiPalestina aliyeuawa katika shambulio la Israel Ukanda wa Gaza.
kichanga hicho kilikuwa na uzani wa 1.4 kg na kiliokolewa kupitia upasuaji wa dharura baada ya waokoaji kubaini kwamba mamake alifariki akiwa na ujauzito wa wiki 30.
Uongozi wa hospitali ya Rafah ulisema kichanga hicho kitakuwa chini ya uangalizi maalum kwa kipindi cha wiki 3 hadi 4 kabla ya kuangalia mchakato wa kuondoka kwake.
“Baada ya kipindi hicho tutaangalia jinsi mtoto huyu ataondoka na atakwenda wapi, iwe kwa familia, kwa wajomba zake au hata babu na bibi. Hapa ndio kuna huruma Zaidi, hata kama mtoto huyo alisalimika, alizaliwa akiwa yatima tayari,” daktari alisema.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, shambulio hilo lililotekelezwa usiku katika mji wa Rafah liliwaua wapalestina wapatao 19.
Kati ya 19 hao walioangamia, 13 wanatoka familia moja.
Mashambulizi ya Israel maeneo hayo yameendelea kwa kisingizio cha kuwasaka wanamgambo wa Hamas tangu Oktoba mwaka 2023.
Inaarifiwa kwamba zaidi ya wakaazi milioni 2 waUkanda wa Gaza, sawa na takriban nusu ya wakaazi wote wametorokea katika mji wa Rafah kutafuta hifadhi dhidi ya mashambulizi ya jeshi la Israel.