Fupa la mjusi mkubwa (mtambaachi) lililogunduliwa karibu na Ziwa Kariba nchini Zimbabwe, limepewa spishi yake baada ya kuonekana lipo tofauti na spishi zilizopo za dinosauri waliowahi kugundulika.
Fupa hilo la mguu wa nyuma wa Mjusi huyo lililogunduliwa likiwa na fupa la paja, hadi kwenye kongo ya mguu, liligunduliwa na Paul Barret kutoka Makumbusho ya mambo ya Kale jijini London.
Fupa hilo lilionekana kuwa na sifa za kipekee uklinganisha na mafupa mengine ya Mijusi wakubwa (Dinosaur), iliyowahi kugunduliwa duniani, alisema Dkt. Kimberley Chapelle.
Na hivyo imebidi kupewa jina lake tofauti nalo ni Musankwa Sayantiensis, kama jina la Kisayansi.
Spishi hiyo ya mijusi mikubwa itakuwa ni ya nne kutokea nchini Zimbabwe.