ZINAZOVUMA:

Fountain Gate na kitayosce wapigwa nyundo na FIFA

Timu ya kitayosce ya ligi kuu pamoja na timu ya...

Share na:

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limezifungia klabu za Kitayosce iliyopanda ligi kuu ya NBC msimu ulioisha na Fountain Gate inayocheza ligi ya Championship usajili wa wachezaji.

Uamuzi huo umefanyika baada ya kocha raia wa Misri aliyewahi kuzifundisha timu hizo kwa nyakati tofauti, Ahmed El Faramawy Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hizo akipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu.

“Baada ya Soliman kushinda kesi, klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini hakuzitekeleza hukumu hizo,” imesema taarifa illiyotolewa na TFF.

Aidha, kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) imezifungia kufanya usajili wa ndani.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya