ZINAZOVUMA:

FIFA yaifungia Yanga kusajili kwa kukiuka kanuni

TFF yaifungia klabu ya Yanga baada ya klabu hiyo kufingiwa...

Share na:

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa kuwa Klabu ya Young Africans (Yanga), imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu (FIFA).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, uamuzi huwo umefanywa na FIFA baada ya Klabu hiyo kukiuka Annex 3 ya kanuni ya uhamisho wa wachezaji (RSTP) ya shirikisho hilo.

Klabu hiyo haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji, katika mfumo wa usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Yanga imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kanuni na kuwasilisha taarifa kwa sekretarieti ya kamati ya nidhamu ya FIFA kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) nalo, limeifungia Klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya