Shirikisho la mpira nchini Ufaransa limekataa ombi la kusimamisha mechi wakati huu wa mwezi wa Ramadhani ili kuwapa nafasi wachezaji waliofunga waweze kufuturu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya waamuzi wa Ufaransa walipokea barua pepe kutoka shirikisho hilo la mpira la Ufaransa FFF kukataza kusimamishwa kwa mechi.
Maamuzi hayo yameibua hisia kubwa kwa wanamichezo na waislamu waliopo nchini Ufaransa wakisema kitendo hicho ni kutoheshimu tofauti za dini za watu ndani ya nchi hiyo.
Mjadala umekua mkubwa zaidi kuhusu namna matendo ya Ufaransa dhidi ya uislamu yanavyoendelea kutishia usalama wa watu wa imani hiyo nchini hapo.
Licha ya maamuzi hayo baadhi ya wachezaji wa kiislamu wataendelea kucheza huku wengine wakichagua kutocheza mpaka baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.