Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei ya ukomo kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa huku kukiwa na ongezeko la bei katika mafuta ya petroli na dizeli.
Bei ya mafuta petroli katika jiji la Dar es Salaam imepanda kutoka Sh2, 736 hadi kufikia Sh3,199 ikiwa ni ongezeko la Sh463 kwa lita.
Bei ya dizeli pia imepanda kutoka Sh2, 544 hadi kufikia Sh 2,935 (ongezeko la 391) huku mafuta ya taa yakipungua kutoka Sh2, 829 hadi Sh2, 668 kwa jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EWURA, bei hizo zinaanza kutumika leo Jumatano Agosti 2, 2023 katika mikoa mbalimbali nchini.
Kupanda kwa bei hizo kumekuja wakati baadhi ya maeneo nchini yakikabiliwa na upungugu wa mafuta ya petroli na dizeli, hali iliyosababisha msongamano wa watu kwenye vituo vya mafuta.