Maelfu ya watu walimiminika jana nje ya Ikulu ya Ankara nchini Uturuki wakisherehekea ushindi wa Rais Recep Erdogan baada ya kutangazwa kumgalagaza mpinzani wake kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana Jumapili ya Mei 28, 2023.
Erdogan (69) amemshinda Kemal Kilicdaroglu kiongozi mkuu wa upinzani wa nchi hiyo kutoka Chama cha RPP kwa asilimia 52 huku Kemal akipata asilimia 48.
Erdogan ambaye anatoka Chama cha AKP, anakuwa Rais wa nchi hiyo ya pili kwa wingi wa watu barani Ulaya, kwa mara nyingine tena hadi mwaka 2028 baada ya kuongoza Taifa hilo toka mwaka 2014.
Hata hivyo kwa upande wa mgombea wa Chama cha upinzani cha RPP, Kilicdaroglu amesema uchaguzi huo haukuwa wa haki na Serikali imeshinikiza matokeo hayo.