Mwanansiasa maarufu nchini Tanzania na aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Willibrod Slaa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi na uhaini, wakili wake amethibitisha.
Wengine waliokamatwa Jumamosi ni Wakili Boniface Mwabukusi na kada wa Chadema, Mpaluka Nyangali maarufu kama ‘Mdude’.
Haya yanajiri baada ya tamko la Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Camillius Wambura la wiki iliyopita akitoa onyo kwa wale ambao wana nia ya kufanya maandamano yenye lengo la kumpindua Rais Samia Suluhu Hassani.
Aidha wakili wa Dkt Slaa mesema mteja wake anatuhumiwa na amehojiwa na polisi kwa makosa ya uchochezi na uhaini hata hivyo hakuna ushahidi wa makosa hayo kwa mujibu wa sheria.