ZINAZOVUMA:

Dkt Slaa aachiwa kwa dhamana

Balozi Dkt Willibrod Slaa ameachiwa kwa dhamana hii Leo katika...

Share na:

Balozi Dkt. Willibrod Slaa ameachiwa kwa dhamana leo katika Kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar es Salaam.

Wakili wake Dickson Matata amesema alipigiwa simu kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam kujulishwa kuwa Balozi Dkt. Willibrod Slaa amefikishwa kituoni hapo.

Taarifa hiyo ilimtaka wakili huyo afike kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kumtolea dhamana kutokana na tuhuma zinazomkabili Dkt Slaa.

Ikumbukwe kuwa juzi Waziri wa Habari, Nape Nnauye alinukuliwa akisema Dkt. Slaa na wenzake, Wakili Mwabukusi na Mdude Nyagali walikamatwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kutoa kauli za kutaka Serikali ipinduliwe na kutoa vitisho vya uhalifu hadharani ikiwemo kuhamasisha Wananchi kubeba silaha ili kupambana na Jeshi la Polisi.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,