ZINAZOVUMA:

Dawa zisiuzwe bila cheti cha Daktari

Katibu Mkuu Wizara ya Afya amewataka wamiliki wa maduka ya...

Share na:

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalage amewataka wamiliki wa maduka ya dawa nchini kufuata utaratibu sahihi wa utoaji dawa kwa wagonjwa kulingana na maelezo ya cheti cha dakitari.

Dkt. Shekalaghe ametoa agizo hilo leo Jijini Tanga wakati wakufungua kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Dkt. Shekalaghe ameeleza kuwa jambo hilo ni la msingi na Serikali wameweka sheria kali kwa mtu atakayekaidi basi atachukuliwa hatua, lakini sasa anawazungumzia wale wanaofanya kwa njia za siri ambao hawajagundulika, hawa wanasababisha tatizo linakuwa kubwa kwa jamii.

“Katika hili napenda kusisitiza wamiliki wa maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na cheti cha daktari”, amesisitiza Dkt. Shekalaghe

Aidha Dkt. Shekalaghe ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kutumia kalamu zao kuweza kutoa elimu kwa wananchi juu ya uelewa wa athari za dawa bila kufata utaratibu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya