ZINAZOVUMA:

Dangote Refinery kuorodheshwa Soko la Hisa la London (LSE)

Dangote Petroleum Refinery imetoa tamko la kampuni hiyo kuorodheshwa kwenye...

Share na:

Mtendaji Mkuu wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote nchini Nigeria Devakumar Edwin, amesema kuwa wanatarajia kuorodhesha kampuni hiyo kwenye Soko la Hisa la Nigeria na Soko la Hisa London.

Taarifa hiyo ya Bw. Devakumar imekuja kama maoni juu ya uamuzi wa kuorodhesha kampuni hizyo katika masoko ya Hisa mawili la Nigeria (NGX) na la London (LSE).

Na Bw. Devakumar amesema kuwa biashara nyingi za Dangote zimeorodheshwa NGX, ila kwa kampuni hii ya mafuta NGX haina uwezo wa kuishughulikia peke yake, hivyo kuna haja ya kuiorodhesha kampuni hiyo kwenye soko jingine la LSE.

Kwani siku chache zilizopita Aliko Dangote mmiliki wa Dangote alinukuliwa akisema kuwa wanatarajia kuorodhesha kampuni ya mafuta hiyo kwenye masoko mawili ya hisa la Nigeria na la London ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Taarufa hiyo imekuja miezi 6 baada ya Dangote kusema nia yake ya kuorodhesha kampuni hiyo kwenye soko la hisa la Nigeria

Tayari baadhi ya kampuni za Dangote zimeorodheshwa katika soko la hisa la Nigeria, ila taarifa zinasema kuwa Soko hilo la hisa linaweza kushindwa kushughulikia kampuni hiyo ya mafuta.

Kampuni hiyo ya mafuta yenye uwezo wa kusafisha laki 6 na nusu kwa siku, itakuwa kubwa barani Afrika na Ulaya, inaweza kufikia kiwango cha juu cha uzalishaji mwaka huu au mwaka ujao.

Na tayari imeshaingia mkataba na Totalenergies wa kupata mafuta ghafi ya WTI kutoka Texas, pipa milioni 2 kila mwezi kwa mwaka mmoja.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya