ZINAZOVUMA:

Dangote kuzindua kiwanda cha kusafisha mafuta

Kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Nigeria kinazinduliwa leo hii na...

Share na:

Kiwanda cha Kusafisha mafuta cha Dangote nchini Nigeria kitaanza kufanya kazi leo Jumatatu Mei 22, 2023 huku kukiwa na matumaini ya kukomesha uhaba wa mafuta unaojitokeza mara kwa mara nchini humo.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kuzindua kiwanda hicho ambacho kinatarajiwa kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika.

Nigeria huaagiza petroli, dizeli na bidhaa nyingne za mafuta kutoka nje kwa sababu mitambo yake ya kusafisha mafuta iliharibika miaka mingi iliyopita.

Serikali ya Raisi anayemaliza muda wake Muhammadu Buhari itashuhudia na kuzindua kiwanda hicho kitakachokua kikisafisha mapipa 650,000 kwa siku.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,