ZINAZOVUMA:

China yatengeneza ndege zake yenyewe

Shirika la ndege la nchini China limekua shirika la kwanza...

Share na:

Shirika la ndege la China Eastern nchini China litakuwa la kwanza kurusha ndege ya abiria iliyotengenezwa na kampuni ya kichina katika safari ya kibiashara. Ndege hiyo ya C919 iliyotengenezwa na kampuni ya Commercial Aircraft Corporation of China (COMAC).

Ndege hiyo inatarajiwa kufanya safari yake ya kwanza ya kibiashara kesho siku ya jumapili saa 4 asubuhi kutokea mji wa Shanghai kuelekea Beijing, ambapo safari hiyo inatarajiwa kuchukua takriban saa mbili na nusu na kufika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing majira ya saa saba na dakika 10 adhuhuri.

Vitu mbalimbali vya ndege hiyo vimebuniwa na makampuni ya kutoka nchini china huku baadhi ya vifaa na vipuri vikiwa vimetengenezwa na makampuni ya magharibi kwa kuwa hawana teknolojia yake. Tayari kampuni mbalimbali zimeweka maombi ya kununua ndege hizo na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2022 kuna maombi ya kununua ndege 1035 kulingana na ripoti ya sayansi na teknolojia inayoandaliwa na Shanghai.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,