ZINAZOVUMA:

China haiko tayari kuiacha huru Taiwan

China imesema ipo tayari kuharibu harakati zozote za Taiwan za...

Share na:

Jeshi la China linasema liko tayari kuharibu harakati za aina yoyote za uhuru wa Taiwan, huku Marekani ikijiandaa kuharakisha uuzaji wa silaha za kujihami kwa demokrasia ya kisiwa hicho kinachojitawala.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi, Kanali Tan Kefei anasema ongezeko la hivi karibuni la mabadilishano kati ya Wanajeshi wa Marekani na Taiwan ni hatua mbaya na hatari yenye kuashiria vita.

Tan anasema Jeshi la ukombozi la Watu wa China linaendelea kuimarisha mafunzo na maandalizi ya kijeshi ili kukabiliana na vikosi vinavyounga mkono uhuru na uingiliaji kutoka nje, akimaanisha mshirika wa karibu wa Taiwan, Marekani.

China inadai kisiwa hicho chenye watu milioni 23 kuwa ni eneo lake na kinapaswa kuwa chini ya udhibiti wake kwa nguvu kama itatakiwa kufanyika hivyo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya