ZINAZOVUMA:

Burkina Faso kutuma majeshi kuisaidia Niger

Bunge la Burkina Faso limeidhinisha azimio la kutuma wanajeshi kwenda...

Share na:

Bunge la mpito nchini Burkina Faso limeidhinisha azimio la kutumwa kwa jeshi nchini Niger ambayo ipo hatarini kushambuliwa na kikosi cha Jumuiya ya ECOWAS ikiwa haitarejesha uongozi kwa Rais Mohammed Bazoum.

Kwa mujibu wa azimio hilo Burkina Faso ambayo pia inaongozwa kijeshi ipo tayari kutuma kikosi chake kwa kipindi cha miezi mitatu, ambacho kinaweza kuongezwa.

Wabunge hao wameazimia kuwa jeshi lake litakwenda nchini Niger pale nchi hiyo itakaposhambuliwa huku lengo likiwa ni kumsaidia jirani yake.

Hatua hii ya Bunge la Burkina Faso inakuja baada ya Jumamosi iliyopita wakuu wa nchi za Niger, Burkina Faso na Mali kutia saini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi.

Tarehe 26 mwezi Julai, jeshi nchini Niger lilimpindua Rais Bazoum kwa madai ya kushindwa kuimarisha usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Jumuiya ya ECOWAS imetishia kutuma jeshi lake, kuhakikisha kuwa Rais Bazoum anarejeshwa madarakani, iwapo uongozi wa kijeshi hautarejesha madaraka kwa uongozi wa Kidemokrasia.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya