ZINAZOVUMA:

Biden ajiandaa kuhudhuria mkutano wa NATO

Raisi wa marekani ajiandaa na ziara ya siku tano ndani...

Share na:

Ikulu ya Marekani imesema kuwa Rais wake Joe Biden anatarajiwa kuondoka wiki ijayo kwa ziara ya siku tano ya mataifa matatu barani Ulaya.

Kituo chake kikuu kitakuwa ni mkutano wa kila mwaka wa NATO mjini Vilnius, Lithuania, ambapo viongozi wa nchi za Magharibi wanapanga kujadili juhudi za kusaidia katika vita vya Ukraine dhidi ya Russia.

Biden, kwanza ataelekea mjini London Jumapili ijayo, katika safari itakayoanza Julai 9 hadi 13, ambapo kwa siku mbili, atakutana na Mfalme Charles na Waziri Mkuu Rishi Sunak, katika juhudi za kuimarisha zaidi, uhusiano wa karibu kati ya mataifa hayo mawili.

Aidha nchi wanachama wa NATO, zikiongozwa na Marekani, zimetuma mabilioni ya dola za kugharamia ununuzi wa silaha nchini Ukraine, lakini mashambulizi ya anga ya Russia yameendelea kusababisha vifo raia wa Ukraine.

Baada ya mkutano wa kilele wa NATO, Biden ataelekea Helsinki, mji mkuu wa Finland, kuadhimisha hatua ya hivi karibuni ya Finland kujiunga na muungano huo wa kijeshi, ulioundwa baada ya Vita vya pili vya dunia, na kukutana na viongozi wa mataifa ya ukanda wa Nordic.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya