ZINAZOVUMA:

Belize yaungana mkono na Gaza dhidi ya Israel

Belize yaungana na Bolivia pamoja na Afrika Kusini kuvunja uhusiano...

Share na:

Serikali ya Belize kutoka bara la Amerika ya Kusini, imevunja uhusiano wa kidiplomasia na Israel.

Hatua hii ya Belize imefuatia baada ya nchi hiyo kuendeleza sera za kizayuni na kimabavu dhidi ya Palestina na Gaza.

Nchi hiyo imeondoa wanadiplomasia wake nchini Israel na kuvunja mahusiano kabisa na taifa hilo la Mashariki ya Kati.

Nchi nyingne zilizovunja uhusiano na taifa hilo la wazayuni ni Bolivia kutoka Amerika ya Kusini na Afrika Kusini kutoka Afrika.

Mbali na kuvunja uhusiano, pia kuna nchi zaidi ya 6 duniani zimeondoa wanadiplomasia wake Israel.

Nchi hizo ni Bahrain, Chad, Chile, Colombia, Honduras, Jordan pamoja na Uturuki.

Pia kuna nchi kadhaa baadhi ya raia wake wamekuwa wakitangaza waziwazi kususia bidhaa za Israel.

India ikishika hatamu kwa matangazo waislamu nchini humo kususia bidhaa za Israel, wakifuatiwa na Indonesia na Uturuki zikitangaza kusuia pia bidhaa za Israel.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya