ZINAZOVUMA:

Bara jipya kupatikana Afrika

Shirika la Anga la Marekani NASA limeonyesha katika utafiti wake...

Share na:

Shirika la Anga la Marekani (Nasa) kupitia utafiti wake mpya uliochapishwa Juni 2023 umeonyesha dalili za kugawanyika mara mbili Bara la Afrika miaka milioni tano ijayo baada ya bonde la ufa lililopo Kenya na Ethiopia kuzidi kuongezeka.

Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa ‘Daily Mail’ wa Uingereza inaonyesha mgawanyiko huo unasababishwa na kusukumwa kwa safu kubwa ya mawe yenye joto kali katika kiini cha dunia.

Pia, utafiti huo unaonyesha baada ya Afrika kugawanyika mara mbili nchi za Tanzania, Kenya, Somalia na sehemu ya Ethiopia itaunda bara jipya litakaloongeza idadi ya mabara kutoka saba hadi nane.

“Wanasayansi wametabiri kwa muda mrefu kwamba Afrika inatazamiwa kugawanyika mara mbili, na kuunda bara jipya ambalo litakuwa na nchi za; Somalia, nusu ya Ethiopia, Kenya na Tanzania,”imeripoti Daily Maily.

Kinachotajwa kuligawa Bara la Afrika ni Bonde la Ufa ambalo lilikuwapo tangu miaka 22 iliyopita, lakini ilianza kuonekana zaidi mwaka 2005 katika eneo la jangwa Ethiopia kabla ya kuongezeka zaidi mwaka 2018 nchini Kenya katika eneo la Maai Mahiu-Narok.

Je ungeulizwa upendekeze jina la Bara jipya ungependekeza jina gani?

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya