ZINAZOVUMA:

Bado tunaendelea na mradi wa Maji Mabalanga Kilindi

Naibu Waziri wa Maji Mha. Kundo Mathew asema wizara yake...

Share na:

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amesema serikali inaendelea na mradi wa maji uliopo kata ya Mabalanga wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga ili kuondokana na adha ya maji kwa wananchi hao wa eneo hilo.

Naibu waziri Amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu suali la Mbunge wa Kilindi Omari Kigua, alilouliza je mhandisi anayejenga mradi wa maji kata ya Mabalanga atakamilisha kazi lini.

Katika majibu ya Mha. Kundo amesema kuwa mradia huo umefikia wastani wa asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika Juni 2024, ukitegemewa utanufaisha wananchi wapatao 6,021 wa Kijiji cha Mabalanga

Aidha ameeleza kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 135, 000, ujenzi wa tanki la kukusanyia maji (Sump well) lenye ujazo wa lita 25000, ujenzi wa vituo 12 vya kuchotea maji, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 6.62, ukaratabati wa machujio ya maji pamoja na ujenzi wa nyumba ya mitambo (Pump house).

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya