Watu 20 wamethibitishwa kufariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama maji kwenye Ziwa Victoria nchini Uganda, ajali iliyotokea maajira ya saa tano asubuhi ya leo.
Boti hiyo ilikuwa na watu 34 na ilikuwa ikitokea kisiwa cha Bukasa kuelekea Entebbe, ambapo polisi wanasema watu 9 wameokolewa, huku chanzo cha ajali hiyo kimethibitishwa kuwa ni upakiaji kupita kiasi na hali mbaya ya hewa
Kwa mujibu wa maofisa wa polisi nchini humo, boti hiyo ambayo ilikuwa imejaa kupita kiasi, ilikuwa pia imebeba magunia ya mkaa, chakula na bidhaa nyengine.
Hii ni ajali ya pili ndani ya wiki moja kutokea katika ziwa Victoria, ya kwanza ikiwa ni Ile ya Mwanza Tanzania iliyohusisha vifo vya watu 13.