Kampuni ya mabasi kutoka nchini Afrika kusini “Mkombe luxury bus” imetangaza safari mpya kutoka Johannesburg mpaka Dar es salaam ikiwa ni miongoni mwa safari ndefu zaidi ya kampuni hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa “Facebook” kampuni hiyo imesema kuanzia Mei 20 2023 miongoni mwa mabasi yake yatasafiri kutoka Johannesburg, Afrika kusini mpaka Dar es salaam Tanzania.
Safari hiyo inatarajiwa kuwa ni ya mwendo wa zaidi ya kilometa 4000 na itapita katika nchi za Botswana, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, na Malawi mpaka kufika Tanzania.
Gharama za usafiri kwa pesa ya Afrika Kusini itakua sawa Dola za kimarekani USD 125 au kwa pesa ya Tanzania itakua sawa na TSH 316,000/-.