ZINAZOVUMA:

ABU DHABI kuzuia Mabasi wakati wa foleni

Ungozi wa Abu Dhabi waweka zuio la mabasi barabarani kwa...

Share na:

Mamlaka ya Abu Dhabi imetangaza marufuku ya magari fulani kwenye barabara kuu kuanzia tarehe 9 Oktoba 2023.

Polisi wa Abu Dhabi, kwa ushirikiano na Kituo cha Usafiri kilichounganishwa, walitumia majukwaa ya kijamii kutangaza marufuku hiyo.

Barabara yenye zuio la vyombo hvyo kupita ni Barabara ya Sheikh Zayed bin Sultan (mwanzo wa Barabara ya Al-Qurram).

Huku zuio hilo likigusa Vyombo vya usafiri vyenye kubeba watu 50 au zaidi ya hapo, kwa mida yenye watumiaji wengi wa barabara asubuhi na jioni.

Marufuku itakuwa inaendeshwa wakati wa muda wa asubuhi kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi na muda wa jioni kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 1:00 usiku.

Hii inafuata juhudi za makusudi za mamlaka ya kudhibiti trafiki na kupunguza ajali zinazosababishwa na magari.

Amri ya Polisi wa Abu Dhabi imewaagiza madereva kutofanya safari wakati wa nyakati zilizopangwa na kufuata mifumo ya trafiki.

Mamlaka imeongeza kuwa itaimarisha ufuatiliaji wa barabara na utekelezaji wa uvunjaji wa sheria kwenye mabasi yanayobeba wafanyakazi ili kufuatilia na kuwakamata wanaokiuka kupitia mifumo ya kidijitali.

Hatua hii inahitajika kuchukuliwa maeneo mbalimbali ya miji ya Afrika Mashariki kama Dar es Salaam na Nairobi, ila kuna hitajio la kuweka mipango inayoendana na mazingira ya miji hiyo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,