Watu wanane wakiwemo watoto wanne wamepoteza maisha kwa kupigwa na shoti ya umeme katika baada ya mvua kubwa kusababisha mafuriko katika makazi ya watu wa hali ya chini karibu na mji wa Cape Town, Afrika Kusini.
Nyumba nyingi katika vitongoji duni vya nje ya mji wa Cape Town vina umeme wa kuunganishwa, ambapo watu huunganisha wenyewe nyumba zao au vibanda kwenye waya za umeme zilizopo.
Waya hizo ni haramu na hatari, lakini zimeenea karibu mahali pote.
Kimbunga ambacho kilipiga eneo la mji wa Cape Town na sehemu kubwa ya mkoa wa Western Cape kwa siku tatu, kilisababisha mito kupasua kingo zake na mafuriko kwenye maeneo ya makazi na barabara kuu.
Zaidi ya wateja 80,000 katika mkoa wote hawakuwa na umeme kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo ilisababisha umeme kukatika.
Lakini baada ya mvua kupungua idadi hiyo ilipungua na kufikia watu 15,000 ambao hawakuwa na umeme.