ZINAZOVUMA:

58 wamekufa wakitaka kwenda mbinguni.

Zaidi ya miili ya watu 58 imefukuliwa huku wengine wakiendelea...

Share na:

Raisi wa Kenya William Ruto amevunja ukimya kuhusu mauaji yaliyofanyika Shakahola ambapo mpaka sasa zaidi ya watu 58 wamepoteza maisha kwa madai ya kuwa wanakufa ili wakakutane na yesu.

Raisi Ruto amesema mchungaji huyo aliewashawishi watu hao kufanya kitendo hicho hastahili kuwa muumini wa dini yoyote bali anastahili kwenda gerezani na kitendo alichokifanya ni cha kigaidi.

Mchungaji huyo aliefahamika kwa jina la Paul Meckenzie wa kanisa la “Good News international” anatuhumiwa kwa kosa la kuwashawishi wafuasi wake zaidi ya 112 kutokula chakula mpaka wafe sababu ndio njia pekee ya kwenda mbinguni.

Mpaka sasa polisi wanaendelea na upelelezi na kufukua makaburi ya watu waliopoteza maisha huku familia za waliopotelewa na ndugu zao zikishinikiza serikali ichukue hatua zaidi kuwapata wale wote wanaohusika.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya