ZINAZOVUMA:

44 wapoteza maisha katika mlipuko, Pakistan

Zaidi ya watu 44 wamepoteza maisha huku 100 wakijeruhiwa katika...

Share na:

Zaidi ya watu 44 wamepoteza maisha katika mlipuko uliotokea nchini Pakistan wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na chama cha Kiislamu.

Zaidi ya watu 100 pia wamejeruhiwa katika mlipuko huo uliotokea kaskazini-magharibi mwa wilaya ya Bajaur, ambapo chama cha kiislamu cha Jamiat Ulema-e-Islam-Fazl (JUI-F) kilikuwa kikifanya mkutano.

Polisi wamesema kwamba wamepata ushahidi unaoonyesha kuwa mlipuko huo ulikuwa ni wa shambulio la kujitoa mhanga.

Shughuli ya uokoaji imekamilika na wote waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini lakini huenda idadi ya vifo ikaongezeka zaidi, kwani watu 15 wako katika hali mbaya.

Sababu ya shambulio hilo bado haijabainika wakati huo vikosi vya usalama vimezingira eneo hilo na uchunguzi zaidi kuhusu mlipuko huo ukiendelea kufanyika.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya