ZINAZOVUMA:

17 wapoteza maisha kwa mvua kubwa Congo

Watu 17 wamepoteza maisha baada ya maporomoko ya udongo yaliyosababishwa...

Share na:

Watu 17 wamepoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo yaliyotokea katika nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maafa hayo yalitokea maeneo ya karibu na kingo za mto Congo, katika mji wa kaskazini wa Lisala, ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Mongala.

Waathiriwa ni pamoja na wanawake saba, wanaume saba na watoto watatu chini ya miaka mitano.

Vifo hivyo vimetokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo kwa muda sasa.

Walioshuhudia walisema nyumba kadhaa kando ya mto huo zimefukiwa chini ya ardhi na baadhi ya wakazi walikuwa wakihangaika kuokoa watu kutoka kwenye vifusi.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,