ZINAZOVUMA:

Zanzibar yampa mwekezaji Bandari ya Malindi

Serikali ya Zanzibar imekabidhi shughuli za uendeshwaji wa bandari ya...

Share na:

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekabidhi shughuli za uendeshaji wa Bandari ya Malindi kwa kampuni ya Kifaransa ya AGL kwa lengo la kuongeza ufanisi katika bandari hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Zanzibar, Joseph Meza amesema hatua hiyo ni kutokana na malalamiko mengi ikiwemo gharama za uletaji wa mizigo kuwa kubwa ikilinganishwa na bandari nyingine.

“Kama sote tunavyojua kumekuwa na malalamiko mengi hasa kwa upande wa Zanzibar kwamba gharama za uletaji mizigo ni kubwa pengine inazidi mara mbili mara tatu ya bandari shindani ambazo tuko nazo, moja ikiwa ni Bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine za Tanzania Bara lakini na majirani zetu ikiwemo Kenya. Gharama za upelekaji mizigo zimekuwa ndogo ukilinganisha na sisi,” amesema.

Aidha, Serikali imetoa uhakika wa utendaji bora wa bandari hiyo ikiwemo kuongezeka kwa zana za utendaji, rasilimali watu pamoja na kuongeza tija katika uendeshaji pindi itakapoendeshwa na mwekezaji huyo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya