ZINAZOVUMA:

Waziri wa Uingereza aishutumu China

Waziri wa Uingereza anaishutumu China kwa kusababisha changamoto kuhusu usalama...

Share na:

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema kuwa China inasababisha changamoto kubwa kuhusu usalama wa dunia na mafanikio, na inaendelea kuwa tishio zaidi.

Katika mkutano wa wiki hii, viongozi wa nchi zenye utajiri wa kiviwanda zaidi duniani G7 wameweka wazi misimamo yao kuhusu masuala yakiwemo ya Indo-Pacific na Taiwan.

Aidha viongozi hao wa nchi zenye utajiri wa kiviwanda zaidi duniani G7 wametuma ujumbe mkali kwa Urusi, huku wakimkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika mkutano wao wa Hiroshima.

Miongoni mwa mahasimu wakubwa waliojadiliwa katika mkutano huo Urusi na China zimeonekana zikichua nafasi kubwa zaidi.

Na katika taarifa zao mbili, viongozi hao wa nchi tajiri zaidi duniani wameweka wazi msimamo wao kuhusu masuala yanayoleta machafuko kama vile lile la Indo-Pacific na Taiwan. Lakini sehemu muhimu zaidi ya ujumbe wao ilikuwa juu ya kile kinachoitwa vitisho vya kiuchumi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya