ZINAZOVUMA:

Wagombea wa Urais wapigwa mabomu ya machozi Madagascar

Wagombea wapinzani wa Urais nchini Madagascar wamepigwa mabomu ya machozi...

Share na:

Maafisa wa usalama nchini Madagascar wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kwa wagombea wa upinzani wa kiti cha urais waliokuwa wakiongoza maandamano katika mji mkuu wa Antananarivo.

Waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP waliona tukio hilo, wakati ambao mivutano ya kisiasa imekua ikiongezeka kabla ya uchaguzi wa rais mwezi ujao.

Wagombea 11 kati ya 13 wa kiti cha Urais walikuwa wametoa wito kwa wafuasi kuandamana katikati ya eneo la Mei 13 kupinga kile walichokielezea kama ni mapinduzi ya kitaasisi yanayo mpendelea Rais aliyepo madarakani Andry Rajoelina.

Lakini maafisa wa polisi waliingia kuutawanya umati wa watu hao kabla haujafika eneo lililopangwa kufanya maandamano.

Rais wa zamani na kiongozi mkuu wa upinzani Marc Ravalomanana, ambaye alikuwa miongoni mwa waandamanaji aliondolewa na kupelekwa eneo salama na walinzi wake.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya