Katika harakati za mabadiliko ndani ya kanisa Katoliki, Vatican imepinga waamini wake kujiunga na FreeMason bila kupepesa.
Kanisa limekuwa likichukulia Freemason kama adui wasiye taka kusuluhishwa nae.
Kanisa lilitoa tamko rasmi lililosainiwa na Papa tarehe 13 mwezi Novemba mwaka huu.
Taarifa hiyo kutoka Vatican lilirejewa azimio la Freemasons la mwaka 1983, ambalo lilisainiwa na Papa Benedicto wa 16.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kanisa kutoa tamko la kukubali kubatia waliobadili maumbile, kubariki ndoa za jinsia moja.
Misimamo hiyo yenye kwenda tofauti na misimamo ya Kanisa ya zamani, imesababisha kuwaengua baadhi ya watu wenye kupinga mabadiliko hayo.
Askofu Joseph E. Strickland wa jimbo la Tyler alisimamishwa, na Askofu Joe Vásquez wa Austin aliteuliwa kushika nafasi iliyoachwa wazi kwa muda.