Nchi ya Ufaransa imetangaza kuwa imesitisha rasmi misaada ya bajeti na maendeleo kwa nchi ya Burkina Faso.
Hatua hii ni baada serikali ya kijeshi ya Burkina Faso kusema itapigana na yeyote atakayejaribu kuwavamia viongozi waliofanya mapinduzi nchini Niger ili kumrejesha Madarakani Rais Mohamed Bazoum
Hatua hii inakuja baada ya muda ambao Jumuiya ya Afrika Magharibi ECOWAS iliwataka Viongozi wa Mapinduzi ya kijeshi nchini Niger kurejesha Utawala wa Kiraia na kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum, kufika kikomo jana Agosti 6, 2023.
Hadi sasa ECOWAS bado haijatoa taarifa kuhusu hatua inayofuata ambayo inajumuisha kuingilia suala hilo.
Hata hivyo jeshi la Niger limetangaza kujiandaa na vita kwa yoyote atakaeingilia au kuvamia nchi hiyo.