ZINAZOVUMA:

TSHISEKEDI: MONUSCO waondoke Congo mwaka huu

Rais Tshisekedi wa DRCongo, avitaka vikosi ya MONUSCO, kutimka nchini...
Rais felix Tshisekedi akihutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York, Nchini Marekani.

Share na:

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuru ia kidemokrasia ya Kongo, atema cheche katika hotuba yake ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA).

Tshisekedi ametaka vikosi vya kulinda amani kutoka Uoja wa mataifa MONUSCO, kujiandaa kuodnoka nchini humo mwishoni mwaka 2023.

Vikosi hivyo vya MONUSCO vimeingia kongo, kulinada amani tangu mwaka 2010.

Hata hivyo vikosi hivyo vilitakiwa kuondoka nchini Kongo mwishoni mwa mwaka 2024.

Rais Tshisekedi amesogeza mbele mpango wa kuondoa vikosi hivyo, kwa mwaka mzima.

Huku akionyesha kuwa sababu ya kufanya hivyo, ni kushindwa kwa vikosi hivyo kulinda amani katika maeneo yake.

Raisi Tshisekedi amesema katika hotuba yake kuwa “Vikosi hivyo na vingine vya amani vimeshindwa kulinda amani kwa zaidi ya miaka 25”

Raisi huyo ameitoa taarifa hiyo, baada ya kuwataka watendaji wa serikali yake kuharakisha mchakato wa vikosi hivyo kuondoka.

Sababu kuu ya uvunjifu wa amani katika ukanda huo tajiri kwa madini mbalimbali Afrika, ni mapigano ya kugombea maeneo yenye madini na rasilimali mbalimbali.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya