Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kituo cha TARI- Hombolo inaendelea na shughuli za Uzalishaji Mbegu za Mtama ambapo kituo kimevuka Malengo ya tani 40 na hivyo hadi sasa kukadiriwa imefika tani 50 hadi 60 na kazi inaendelea.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa kituo cha TARI- Hombolo Dkt. Joel Meliyo wakati akitoa tathimini juu ya hali ya Uzalishaji wa Mbegu za Mtama katika Mashamba ya kituo hicho Machi 28, 2023 Mkoani Dodoma.
Miongoni mwa aina ya Mbegu zilizozalishwa ni Macia yenye uwezo wa kustahimili hali ya mabadiliko ya nchi kwa kuwa haziitaji mvua nyingi na zina mavuno Mengi.
Kufuatia Hatua Hiyo Mkurugenzi Dkt. Meliyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imetoa fedha kuwezesha Uzalishaji kupitia Mradi wa “Post Covid recovery”.