ZINAZOVUMA:

Niger yatangaza serikali ya mpito

Jenerali Abdourahmane Tchiani ametangaza serikali mpya ya mpito licha ya...

Share na:

Jenerali Abdourahmane Tchiani, aliyeongoza mapinduzi Niger ametangaza baraza jipya la serikali ya mpito licha ya kuwepo wito wa kumtaka amrejeshe madarakani Rais Mohamed Bazoum.

Serikali hiyo mpya inaundwa na mawaziri 21, wakiwemo mawaziri wawili wa serikali iliyopita na itaongozwa na Waziri Mkuu wa muda Lamine Zeine Ali Mahamane, ambaye pia ataongoza Wizara ya Uchumi na Fedha.

Aliyekuwa mkuu wa wafanyikazi Luteni Jenerali Salifou Mody, ambae ni naibu wa Jenerali Tchiani, ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa.

Kanali Meja Abdourahmane Amadou, ambaye amekuwa akitoa taarifa nyingi za jeshi hilo tangu mapinduzi ya Julai 26, ameteuliwa kuwa Waziri wa Vijana na Michezo.

Tayari jeshi hilo limewataja wakuu wapya wa kijeshi na kuwafuta kazi maafisa wengi wakuu wa serikali waliohudumu katika utawala wa Bazoum.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya