ZINAZOVUMA:

Mwanzilishi wa Telegram akamatwa Ufaransa

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa...

Share na:

Mrusi Pavel Durov mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Telegram, amekamatwa nchini Ufaransa kwa makosa yahusuyo mwenendo wa mtandao wake.

Serikali ya Urusi iliweka wazi ombi lake la kumpatia raia wakehuyo, msaada wa kibalozi bila mafanikio kutoka kwa serikali ya Ufaransa.

Pavel Durov alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Le Bourget kaskazini mwa Paris, akiwa kwenye ndege binafsi siku ya jumamosi akitokea Azerbaijan.

Durov alikamatwa kwa tuhuma za mtandao wa Telegram kutumika na makundi mbalimbali ya kigaidi katika kuwasiliana.

Durov amekamatwa kwa kushindwa kuchukua hatua za kupunguza matumizi ya jukwaa lake kwa madhumuni ya uhalifu duniani.

Shirika la OFMIN la Ufaransalinalojihusisha na kuzuia vurugu dhidi ya watoto, lilitoa kibali cha kukamatwa kwa Durov.

Kukamatwa huko ni sehemu ya uchunguzi wa awali juu ya makosa yanayoshukiwa kufanyika kupitia mtandao huo kama usafirishaji wa dawa za kulevya, uhalifu mwingine wa kupangwa na kukuza ugaidi.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Telegram anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya jumapili nchini Ufaransa.

Endelea Kusoma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya