ZINAZOVUMA:

Marekani yatangaza kusitisha msaada Gabon

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametangaza kuwa nchi...

Share na:

Marekani imesema kwamba itasitisha misaada yake kwa nchi ya Gabon baada ya jeshi kuchukua madaraka mwezi uliopita nchini humo.

Katika taarifa yake Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema serikali yake imesitisha baadhi ya programu za usaidizi zinazonufaisha serikali ya Gabon huku ikitathmini uingiliaji kati usio wa kikatiba uliofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo.

Hata hivyo, Blinken amesema kuwa Marekani inadumisha operesheni za kidiplomasia na kibalozi katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta ya Afrika ya Kati, na kwamba hatua ya kusitisha misaada kwa sasa ni ya muda.

Awali maafisa wa Marekani walisema kwamba msaada wa Marekani ulikuwa mdogo kwa serikali ya Gabon, iliyokua ikiendeshwa na familia ya Bongo kwa zaidi ya nusu karne.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya