Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) imesitisha ratiba zake za mwezi Juni, kutokana na uhaba wa fedha katika taasisi hiyo.
Sababu kubwa ya uhaba huo wa fedha ni kuto kufika kwa wakati michango ya nchi wanachama, ambayo ndio huwa inaendesha shughuli zote za mahakama hiyo.
Mahakama hiyo litoa taarifa rasmi kwa umma na wadau wenye kesi tarehe 27 mwezi Mei, kuwa hakutakuwa na vikao vya kesi zinazosikilizwa kwa mara ya kwanza mwezi Juni.
“Changamoto hii inazuia kazi ya msingi ya Mahakama hii hasa ya kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya kesi zilizoletwa”.
“Na hadi sasa kuna kesi zilizowekwa kwenye msururu wa kusikilizwa zaidi ya 200 katika mahakama hii” iliendelea taarifa hiyo.
Mbali na Mahakama hiyo kusitisha shughuli zake, Bunge la Afrika Mashariki (EALA) limekuwa likipitia changamoto za namna hii kwa kukosa fedha za kujiendesha.
Hali iliyofanya Bunge hilo kuleta shauri la kuweka pingamizi kwa wanachama wasioleta michango yao kwa wakati.