ZINAZOVUMA:

Kampuni ya Kipakistan yapata Kandarasi NEOM

Mji wa Neom nchini Saudi Arabia, unaotarajiwa kuwa na ...
Ramani ya eneo utakapojengwa Mji wa Neom nchini Saudi Arabia.

Share na:

Kampuni ya kutoka Pakistan imepata kandarasi ya dola Milioni 12 za Marekani katika mradi wa Mji wa Neom.

Makamu wa Raisi wa Maendeleo na Biashara, wa National Engineering Services Pakistan (NESPAK), ameeleza kuwa mradi huo utaanza muda si mrefu.

Na tayari kampuni yake ilitia saini makubaliano, kusimamia ujenzi wa baadhi ya miundombinu ya umeme katika mradi huo .

Kandarasi ya NESPAK itahusisha maeneo ya Ghuba ya NEOM, Mlima wa Neom na Awamu ya pili ya Neom.

Taarifa zote hizi alizisema makamu wa raisi wa maendeleo ya biashara wa kampuni ya NESPAK Bw. Ahmad Said.

Mradi wa NEOM ni wa kimkakati nchini Saudi Arabia, umesanifiwa kuwa ni wa kipekee katika uwekezaji wa nchi hiyo.

Trojena (kushoto) na Oxagon kulia, maeneo mawili yanayotarajiwa kujengwa kaskazini na kusini mwa Mji wa Neom

Mji wa Neom unatarajiwa kuwa ni mji usiozalisha hewa ukaa “Zero Carbon”, kutokana na nishati safi inayotarajiwa kutumika.

Urefu wake utakuwa Kilomita 170, upana wa mita 200, na eneo la kilomita 34 za mraba.

Mahitaji yote ya magari yataondolewa kwa kuweka mahtaji muhimu yote ndani ya mwendo wa kutembea dakika 5.

Na matembezi yote ya umbali mrefu yatakuwa kwa treni ya mwendo kasi.

Pia upande wa kusini utajengwa mji “Oxagon” unaoelea baharini, utakuwa bandari na viwanda vya kisasa.

Huku Trojena ikiwa upande wa kaskazini mahsusi kwa kuvinjari, hasa mchezo maarufu wa kuteleza kwenye theluji “Skiing”.

Na pia inatarajiwa kuwa na hoteli inayopaa angani, huku ikijitegemea kwa kila kitu, katika mahitaji ya vyumba vya hoteli iliyopewa jina la Nimbus.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya